Kanuni za Barabara ni jumla ya sheria na ushauri wa namna ya kutumia barabara zetu. Kanuni hizi zinahusisha sheria ya barabarani na desturi ya uendeshaji mzuri. Migogoro ni kawaida kwenye mfumo wowote wa barabara, lakini iwapo wote tutafuata kanuni zilezile tunapokuwa barabarani, na kutenda katika namna ya kujali na kuwajibika kwa wengine, usafiri wetu barabarani utakuwa wa salama na usio wa mashaka. Kanuni za Barabara zitawafaa hasa madereva wanafunzi, kwani wanahitaji kuzifahamu ili kufaulu mafunzo yao ya udereva, lakini tunashauri kuwa, hata kama umekuwa ukiendesha gari kwa muda fulani, soma Kanuni hizi ili kujikumbusha maarifa yako kuhusu sheria. Pia Kanuni za Barabara zinajumuisha ushauri unaofaa kwa watembea kwa miguu, waendesha baiskeli na watumiaji wengine wa barabara wanaoweza kudhurika – pia wao wana wajibu wa kuendesha katika
namna ya kujali na umakini.Tunawaomba watumiaji wote wa barabara kujifunza Kanuni za Barabara
na kufuata ushauri uliotolewa. Iwapo kila mmoja atafanya hivi, usafi ri wa barabarani utakuwa wa salama na wa kufurahisha zaidi.
Askari wa usalama barabarani. |
Uwe katika hali nzuri. Unatakiwa kuwa katika hali nzuri kuweza kuitumia barabara kwa usalama. Iwapo hutakuwa katika hali nzuri, usiendeshe. Tafuta msaada iwapo unatakiwa kwenda mahali fulani.
Usitumie barabara iwapo unatumia pombe au dawa za kulevya kiasi cha kukufanya kutojiweza. Iwapo unatumia dawa muombe ushauri daktari wako kama unaweza kuendesha.
Wajibika. Una wajibu wa kufanya jitihada yoyote kuepuka kufanya kitu chochote kinachoweza kuleta madhara kwa wengine. Hivi hujumuisha vitu vinavyojulikana kuwa vya hatari, mfano kuendesha kwa kasi, kunywa pombe halafu ukaendesha, na kulipita gari jingine kwenye kona.
Kuwa makini. Utumiaji salama wa barabara unahitaji umakini wako mkubwa, kwa dereva au mtembea kwa miguu. Usiwaruhusu wengine wakuvuruge.
Kuwa mtulivu na mvumilivu. Epuka kuwa na hasira kuhusu tabia mbaya ya wengine. Usijaribu kuwaadhibu. Kuwa mvumilivu kwenye foleni, na usifanye fujo kwa kujaribu kuwapita walio mbele yako. Usitumie barabara iwapo una hasira, umesisimuliwa sana au kufadhaishwa sana na jambo fulani.
Wasaidie wengine. Iwapo kila mmoja atafuata sheria na kuwasaidia wengine kutapunguza kuchelewa. Ubinafsi huharibu mambo kwa kila mtu na inaweza kuwa hatari.
Walinde walio katika hatari. Una wajibu wa kuwalinda na kuwasaidia wazee, walemavu, na watoto. Madereva wa magari lazima wawe makini zaidi wanapochangia barabara na wale wenye uwezo mdogo wa kujikinga na majeruhi – hawa ni pamoja na watembea kwa miguu, waendesha baiskeli na waendesha pikipiki.
Usipige kelele zisizo na sababu. Kelele kupita kiasi huvuruga na
kuchosha. Iwapo unaendesha gari kumbuka kuwa honi hutumika tu
wakati wa dharura.
Basi likiovertake eneo ambalo halitakiwi kufanya hivyo. |
0 comments:
Post a Comment