Zingatia Wajibu. USIFANYE tabia yoyote inayoweza kuwa ya hatari kwako au watumiaji wengine wa barabara.Tumia njia ya watembea kwa miguu. Iwapo kuna njia ya watembea kwa miguu itumie. Usitembee karibu na ukingo wa barabara mgongo wako ukiwa upande wa barabara. Usitembee barabarani isipokuwa unapokuwa umehakikisha kuwa ni salama kufanya hivyo.Tembea upande wa kulia. Endapo kuna njia ya watembea kwa miguu, pita upande wa kulia wa barabara ili uweze kuyaona magari yanayokuja. Inapowezekana, hususan kwenye barabara nyembemba au kwenye mwanga mdogo, tembea kwenye mstari mmoja na wengine. Uwe mwangalifu sana kwenye kona kali
za upande wa kulia. Jiwezeshe kuonekana kwa urahisi. Vaa au beba kitu ambacho mara zote kitakusaidia kuonekana. Vitu vinavyong’aa au kuakisi mwanga vitakusaidia kuonekana kunapokuwa hakuna mwanga wa kutosha mchana. Wakati wa usiku tumia vitu vinavyoakisi vinavyoweza
kuonekana katikamwanga.Kutembea na watoto. Usimruhusu mtoto mdogo atembee peke yake
kwenye njia ya watembea kwa miguu au barabarani. Unapotembea na watoto, tembea katikati yao na barabara ukiwa umeshika kwa nguvu mikono yao.
Kutembea kwenye kundi. Iwapo kundi la watu linashiriki kwenye matembezi yaliyopangwabarabarani, watembea upande wa kulia. Waandaaji wahakikishe kuna walinzi mbele na nyuma waliovaa nguo
zinazong’aa katika mwanga wa mchana na nguo zinazoakisi wakati wa giza.
0 comments:
Post a Comment