ABOUT BRCC

ABOUT BRCC
IT WAS AWESOME



Jumatano ya wiki iliyopita ndio liliibwa hili gari aina ya BMW lisilopenya risasi ambalo huwa linakuwepo kwenye msafara wa Rais Kenyatta, na taarifa ya Ikulu ilisema liliibwa wakati dereva wake ambae ni askari alikua akielekea kwenye makazi ya Polisi Nairobi, njiani akasimamishwa na watu waliokua na AK 47 wakamtupa mtaroni baada ya kumvua nguo na kukimbia nalo. Taarifa mpya ambayo inaripotiwa na ripota wa TZA Kenya Julius Kepkoich inasema gari hili limepatikana kwenye mji wa Tororo Uganda na tayari limepelekwa Kampala baada ya msako uliofanywa na Polisi na kumkamata mshukiwa mmoja hotelini mjini Bungoma. Kikosi cha Polisi wa Flying squard kikishirikiana na Interpol walivuka boda na kuingia mji wa Tororo Uganda walikohisi kwamba ndiko kulikopelekwa gari hilo. Polisi wanamshikilia Nelson Topicho aliyekamatwa Bungoma na anatarajiwa kurejeshwa Nairobi ili kuhojiwa zaidi ambapo kikosi kingine cha Nakuru Kenya kinamshikilia Agrey Odhiambo anaetuhumiwa kukarabati gari lililoibwa na kumiliki bunduki huku Nairobi wakitarajiwa kumuhoji upya dereva wa Ikulu David Muchui.

Source : Millardayo.com

0 comments:

Post a Comment

 
© Bongo Ride - All Rights Reserved. Developed by Classic Sean and Kicbjamii
Top