ABOUT BRCC

ABOUT BRCC
IT WAS AWESOME

Kituo kipya cha daladala kilichopo eneo la Migombani jirani na jengo la mawasiliano kitakachochukua nafasi ya kituo cha ubungo. Kinatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwezi huu baada ya kukamilika sehemu kubwa.



Ujenzi wa kituo hicho ambao ulianza mwaka jana umekamilika kwa asilimia kubwa huku manispaa ya kinondoni ikiwa na lengo la kuongeza nafasi kwaajili ya maeneo ya wafanya biashara. Hayo yamesemwa na meya wa manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda baada ya kikao cha baraza la madiwani wa manspaa hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Moja ya majengo ya kisasa yatakayotumika kama ofisi.



Mwenda alisema kuwa wameona ni vyema kuongeza eneo kwaajili ya wafanyabiashara ili kuongeza vyanzo vya mapato vya manispaa hiyo. “mwisho wa mwezi huu kituo ndio kitaanza kutumika rasmi, kwasababu sasa hivi tunaongeza sehemu ya wafanyabiashara” alisema Mwenda 

Maeneo ya kupumzika abiria wakiwa wanasubiri usafiri.






 Imeandikwa na Katuma Masamba.

2 comments:

  1. Tanzania inakua...

    ReplyDelete
  2. Tukitunze tu, maana wabongo kwa uharibifu hatujambo.

    ReplyDelete

 
© Bongo Ride - All Rights Reserved. Developed by Classic Sean and Kicbjamii
Top