Kituo
kipya cha daladala kilichopo eneo la Migombani jirani na jengo la mawasiliano
kitakachochukua nafasi ya kituo cha ubungo. Kinatarajiwa kuanza kutumika
mwishoni mwa mwezi huu baada ya kukamilika sehemu kubwa.

Ujenzi
wa kituo hicho ambao ulianza mwaka jana umekamilika kwa asilimia kubwa huku
manispaa ya kinondoni ikiwa na lengo la kuongeza nafasi kwaajili ya maeneo ya
wafanya biashara. Hayo yamesemwa na meya wa manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda baada ya kikao cha baraza la madiwani wa manspaa hiyo kilichofanyika
jijini Dar es Salaam.
