Sunday, January 12, 2014

TOYOTA LANDCRUISER DIESEL REVIEW

Vehicle Style: Large SUV
Engine / trans: 4.5 litre twin-turbo V8 diesel / 6spd sports auto
Power / torque: 195kW @ 3400 RPM / 650Nm @ 1600 RPM
Fuel Economy claimed: 10.3 lt/100km | tested: 13.6 lt/100km
 
Would anyone dispute the credentials of Toyota’s LandCruiser as an off-road vehicle?
 With over half a century of R&D behind it, the LandCruiser range has rightfully built a reputation for tough-as-nails capability.

Usalama barabarani kwa waenda kwa miguu

Zingatia Wajibu. USIFANYE tabia yoyote inayoweza kuwa ya hatari kwako au watumiaji wengine wa barabara.Tumia njia ya watembea kwa miguu. Iwapo kuna njia ya watembea kwa miguu itumie. Usitembee karibu na ukingo wa barabara mgongo wako ukiwa upande wa barabara. Usitembee barabarani isipokuwa unapokuwa umehakikisha kuwa ni salama kufanya hivyo.Tembea upande wa kulia. Endapo kuna njia ya watembea kwa miguu, pita upande wa kulia wa barabara ili uweze kuyaona magari yanayokuja. Inapowezekana, hususan kwenye barabara nyembemba au kwenye mwanga mdogo, tembea kwenye mstari mmoja na wengine. Uwe mwangalifu sana kwenye kona kali 
za upande wa kulia. Jiwezeshe kuonekana kwa urahisi. Vaa au beba kitu ambacho mara zote kitakusaidia kuonekana. Vitu vinavyong’aa au kuakisi mwanga vitakusaidia kuonekana kunapokuwa hakuna mwanga wa kutosha mchana. Wakati wa usiku tumia vitu vinavyoakisi vinavyoweza 
kuonekana katikamwanga.Kutembea na watoto. Usimruhusu mtoto mdogo atembee peke yake 
kwenye njia ya watembea kwa miguu au barabarani. Unapotembea na watoto, tembea katikati yao na barabara ukiwa umeshika kwa nguvu mikono yao.
Kutembea kwenye kundi. Iwapo kundi la watu linashiriki kwenye matembezi yaliyopangwabarabarani, watembea upande wa kulia. Waandaaji wahakikishe kuna walinzi mbele na nyuma waliovaa nguo 
zinazong’aa katika mwanga wa mchana na nguo zinazoakisi wakati wa giza.

Usalama Barabarani


Kanuni za Barabara
 ni jumla ya sheria na ushauri wa namna ya kutumia barabara zetu. Kanuni hizi zinahusisha sheria ya barabarani na desturi ya uendeshaji mzuri. Migogoro ni kawaida kwenye mfumo wowote wa barabara, lakini iwapo wote tutafuata kanuni zilezile tunapokuwa barabarani, na kutenda katika namna ya kujali na kuwajibika kwa wengine, usafiri wetu barabarani utakuwa wa salama na usio wa mashaka. Kanuni za Barabara zitawafaa hasa madereva wanafunzi, kwani wanahitaji kuzifahamu ili kufaulu mafunzo yao ya udereva, lakini tunashauri kuwa, hata kama umekuwa ukiendesha gari kwa muda fulani, soma Kanuni hizi ili kujikumbusha maarifa yako kuhusu sheria. Pia Kanuni za Barabara zinajumuisha ushauri unaofaa kwa watembea kwa miguu, waendesha baiskeli na watumiaji wengine wa barabara wanaoweza kudhurika – pia wao wana wajibu wa kuendesha katika 
namna ya kujali na umakini.Tunawaomba watumiaji wote wa barabara kujifunza Kanuni za Barabara 
na kufuata ushauri uliotolewa. Iwapo kila mmoja atafanya hivi, usafi ri wa barabarani utakuwa wa salama na wa kufurahisha zaidi.
Askari wa usalama barabarani.
 
© Bongo Ride - All Rights Reserved. Developed by Classic Sean and Kicbjamii
Top